Nauli za SGR, daraja la kawaida
| Safari | Mtu mzima | Mtoto 4–12 | Chini ya miaka 4 |
|---|---|---|---|
| Dar es Salaam – Morogoro | TZS 13,000 | TZS 6,500 | TZS 0 |
| Dar es Salaam – Dodoma | TZS 31,000 | TZS 15,500 | TZS 0 |
Nauli hizi ziliwekwa na Bodi ya LATRA na kutangazwa tarehe 10.06.2024. Ni za kwenda tu, kwa daraja la kawaida (Economy).
Jinsi nauli inavyohesabiwa
LATRA ilipanga nauli kwa kilomita: TZS 69.51 kwa kila kilomita kwa mtu mzima (zaidi ya miaka 12) na TZS 34.76 kwa mtoto wa miaka 4 hadi 12. Dar es Salaam hadi Dodoma ni kilomita 444: 444 × 69.51 ≈ TZS 30,862, nauli iliyotangazwa ni TZS 31,000. Uamuzi wa LATRA unahusu njia hadi Makutupora, baada ya Dodoma ambacho ni kituo cha mwisho cha abiria; kwa vituo vyote hadi huko nauli ya mtu mzima ni kati ya TZS 1,000 na TZS 37,000, ya mtoto kati ya TZS 500 na TZS 18,500.
Business na Royal
Nauli za Business na Royal zinawekwa na TRC na zinaonekana kwenye mfumo wa tiketi unapochagua treni na behewa. Ziangalie hapo siku unayokata tiketi.
Reli ya kati: Dar es Salaam – Arusha (Deluxe)
| Daraja | Mtu mzima (13+) | Mtoto (4–12) |
|---|---|---|
| Daraja la tatu | TZS 18,700 | TZS 9,350 |
| Daraja la pili, kukaa | TZS 26,700 | TZS 13,350 |
| Daraja la pili, kulala | TZS 44,400 | TZS 22,200 |
Mtoto wa miaka 0–3 halipi. Nauli za njia nyingine za reli ya kati (Kigoma, Mpanda) unazipata kwa kitufe cha “Pata nauli” kwenye eticketing.trc.co.tz. Treni za reli ya kati
Treni ya mjini Dar es Salaam
| Njia | Mtu mzima | Mwanafunzi |
|---|---|---|
| Dar es Salaam – Pugu | TZS 600 | TZS 100 |
| Dar es Salaam – Ubungo | TZS 400 | TZS 100 |
Njia na siku za treni ya mjini: treni za reli ya kati
Maswali kuhusu nauli
Nauli ya SGR Dar es Salaam hadi Morogoro ni kiasi gani?
TZS 13,000 kwa mtu mzima na TZS 6,500 kwa mtoto wa miaka 4–12, daraja la kawaida.
Nauli ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma ni kiasi gani?
TZS 31,000 kwa mtu mzima na TZS 15,500 kwa mtoto, daraja la kawaida.
Je, watoto hulipa nauli ya SGR?
Mtoto wa miaka 4 hadi 12 analipa nusu ya nauli ya mtu mzima. Mtoto chini ya miaka 4 halipi, lakini taarifa zake zinaingizwa kwenye mfumo.